Psalms 103:8-17

8 a Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema;
si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.
9 bYeye hatalaumu siku zote,
wala haweki hasira yake milele,
10 cyeye hatutendei kulingana na dhambi zetu
wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.
11 dKama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana,
ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;
12 ekama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.
13 fKama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,
ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha;
14 gkwa kuwa anajua tulivyoumbwa,
anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi.
15 hKuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani,
anachanua kama ua la shambani;
16 iupepo huvuma juu yake nalo hutoweka,
mahali pake hapalikumbuki tena.
17 jLakini kutoka milele hata milele
upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao,
nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:
Copyright information for SwhNEN